U-13 kwenda Ubeligiji

Mshambuliaji wa Serengeti Boys, Abdul Hamis Suleiman akipiga shuti mbele ya kipa wa Niger

Timu ya Taifa Vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U13) inatarajiwa kushiriki michuano ya vijana itakayozikutanisha timu za vijana za nchi zaidi ya 10 kutoka mataifa mbalimbali nchini Ubeligiji mwezi Agosti, 2018.

TFF inaanda utaratibu sahihi wa kupata kikosi cha timu ya Taifa kwa vijana wenye umri huo ili kuweza kujiandaa na michuano hiyo ya vijana.

Kwa kuanzia kutachezwa mechi kati ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 kutoka Tanzania Bara dhidi ya vijana wa Zanzibar katika siku za hivi karibuni ili kutoa nafasi kwa waalimu kuchagua wachezaji wenye vipaji watakaounda kikosi hicho cha U13.

One Comment

  1. Pingback: U-13 kwenda Ubeligiji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *