Twiga Stars yaingia kambini kujiwinda na She-Polopolo ya Zambia

Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini katika Hostel za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa) kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataia Afrika kwa Wanawake AFCON 2018 nchini Ghana.

Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8, 2018 jijini Lusaka nchini Zambia.

Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo wa Wanawake Afrika.

One Comment

  1. Pingback: Twiga Stars yaingia kambini kujiwinda na She-Polopolo ya Zambia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *