Robo Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) kuchezwa mwisho wa mwezi

Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi Machi katika viwanaj vine tofauti nchini.

Ijumaa Machi 30, 2018 kutakua na mchezo mmoja katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ambapo wenyeji Stand United watawakaribisha Njombe Mji saa 10:00 jioni.

Machi 31, 2018 kutakua na michezo miwili, Tanzania Priosns watakua wenyeji wa JKT Tanzania saa 8:00 mchana uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku saa 2:00 usiku Azam FC watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Chamazi Compex, Dar es salaam.

Jumapili Aprili Mosi, 2018 kutakua na mchezo mmoja, Singida United watakua wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Namfua mjini Singida Aprili Mosi, 2018 mchezo utakaonza saa 10:00 jioni.

One Comment

  1. Pingback: Robo Fainali Kombe la Shirikisho (ASFC) kuchezwa mwisho wa mwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *