Ngorongoro Heroes kujipima na Morocco, Msumbuji wikiend kabla ya kuwavaa DR Congo

Kikosi cha Serengeti kilichoanza pambano ( Picha/ Hisani CAF )

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Morocco na Msumbuji kabla ya kuwavaa DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana (AFCON U20).

Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji Jumatano Machi 21, 2018 michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili mbili jijini Kinshansha Congo DR.

Ngorongoro Heroes imeingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach iliyopo Mbweni ambapo inajiandaa na michezo hiyo miwili ya kirafiki na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 20.

One Comment

  1. Pingback: Ngorongoro Heroes kujipima na Morocco, Msumbuji wikiend kabla ya kuwavaa DR Congo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *