Westbrom yaichapa Man UTD, Liverpool yashinda

Ligi Kuu ya Soka nchini Uingereza ‘Premier League’ imeendelea kutimua vumbi Jumapili hii kwa michezo miwili.

Katika dimba la The Hawthorns, klabu ya Westbrom imeweza kujiandika ushindi wa kukumbukwa wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United.

 Katika mchezo huo, Mshambuliaji nyota mwenye asili ya kihispania Juan Mata alijiona akipata kadi nyekundu baada ya kuonywa mara mbili na muamuzi wa pambano hilo Mike Dean kutokana na rafu aliomchezea Darren Fletcher.

Pengo hilo la mchezaji mmoja kwa Manchester united liliwapa nguvu Westbrom na kuweza kujipatia bao pekee na la ushindi kwenye dakika ya 67 kupitia mshambuliaji Jose Rondon.

Katika Dimba la Selhurst Park, Klabu ya Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace.

 Crystal Palace walikuwa wakwanza kuziona nyavu kwenye dakika ya 49 kupitia kiungo Joseph Ledley, huku kiungo Mshambuliaji wa Liverpool James Milner akipokea kadi nyekundu baada ya kuonywa mara mbili na muamuzi Andre Marriner kwenye dakika ya 62.

Liverpool ilipata bao la kusawazisha kwenye dakika ya 72 kupitia kiungo mshambuliaji Robert Firmino kabla ya mshambuliaji Christian Benteke kupachika bao la ushindi kwenye dakika ya 90 kwa mkwaju wa penati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *