Rafa Benitez arudi tena kwenye EPL

Baada ya kumtimua kocha Steven Mclaren alieyeinoa klabu hio kwa takribani miezi 9, Klabu ya Newcastle United imemteua Rafa Benitez kuwa kocha mpya wa klabu hio inayo shiriki Ligi Kuu nchini Uingereza “Premier League”.

Newcastle ilifikia maamuzi hayo ya kumtimua Mclaren baada ya matokeo mabovu ambapo illiona timu hio ikishinda mechi sita kati ya echi 28 walizocheza.

Benitez ambaye amewahi kufundisha klabu kubwa duniani kama Chelsea, Inter Milan, Liverpool pamoja na Real Madrid amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuinoa klabu hio ya Newcastle.

Rafa Benitez

Rafa Benitez

Benitez atakuwa na kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha klabu hio inabaki kwenye Ligi Kuu kwani Newcastle inashika nafasi ya 19 ikiwa na pointi 24 huku zikisalia mechi 10 kufikia tamati ya msimu huu wa 2015/16.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *