Chicharito ashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka

Chicharito

Mshambuliaji wa klabu ya Bayer Leverkusen, Javier Henandez ‘Chicharito’  jana usiku alinyakua tuzo ya mchezaji bora wa soka wa ukanda wa Amerika Kaskazini wa mwaka 2015.

Chicharito amekuwa katika kiwango bora tangu atue Bayer Leverkusen kwa mkopo. Alichaguliwa mchezaji bora wa Ligi ya Ujerumani mwezi Novemba.

Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Mexico amefunga mabao 11 katika mechi 14 za Bundesliga na pia amefumania nyavu mara 5 katika mechi sita za ligi ya Manbingwa msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *