Bayern yaanza mwaka kwa ushindi dhidi ya Hamburger

Bayern Munich imeweza kuendeleza mnyororo wao wa ushindi usiku wa jana baaada ya kuichapa Hamburger SV kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Volkspark stadion wakati ligi kuu chini Ujerumani ikirejea kutoka kwenye mapumziko ya takribani mwezi mmoja.

Bayern ilipata goli la kwanza kwa mkwaju wa penati uliowekwa nyavuni na Robert Lewandowski kwenye dakika ya 37 baada ya mshabuliaji wa Kijerumani Thomas Muller akiangushwa kwenye dimba la hatari na kipa wa Hamburger Rene Adler.

Robert Lewandowski [Photo: @FCBayernEN]

Robert Lewandowski [Photo: @FCBayernEN]

Hamburger iliweza kusawazisha bao hilo kwenye dakika ya 53 kwa ‘free kick’ nzuri iliopigwa na kiungo wa kijerumani Aaron Hunt ambapo mpira huo ulimgusa kiungo wa kihispania Xabi Alonso wakati akijaribu kuuzuia.

Lewandowski aliendelea kuonyesha moto wake alipofunga bao lake la pili kwenye dakika ya 61 akiunganisha shuti kutoka kwa Thomas Muller na kujiandikia bao lake la 17 kwenye ligi msimu huu.

Angalia mabao yote ya mchezo huo hapa:

Mechi za Jumamosi hii kwenye bundesliga:
Ingolstadt v Mainz
Hoffenheim v Bayer Leverkusen
Hertha Berlin v Augsburg
Hannover 96 v Darmstadt
FC Koln v Stuttgart
Borussia Monchengladbach v Borussia Dortmund

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *