Zanaco, APR zashikilia tiketi ya Yanga makundiLigi ya Mabingwa Afrika

IMG_2592_20161101220441710

Shirikisho la soka barani Afrika, CAF limetoa ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwapangia wawakilishi wa Tanzania Bara, Yanga kuanza katika raundi ya awali dhidi ya mabingwa wa Comoro, Ngaya de Mbe.

Ikifanikiwa kuwatoa Wacomoro , Yanga itacheza na mshindi wa pambano baina ya Zanaco ya Zambia na APR yA Rwanda kusaka tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hio iliyotanuliwa kwa kushirikisha makundi manne  badala ya mawili kama ilivyokuwa mwaka huu.

Yanga itaanzia ugenini dhidi ya Ngaya de Mbe kabla ya kurudiana na Wacomoro jijini Dar wakati huo APR na Zanaco zikipambana katika mechi za mtoano za nyumbani na ugenini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *