Zahoro Pazi ruksa kuchezea Mbeya City

Zahoro Pazi

Zahoro Pazi

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Zahoro Pazi anaweza kuanza kuitumikia timu yake mpya ya Mbeya City baada ya kupata kibali cha Uhamisho wa leseni ya Kimataifa (ITC) hii leo.

Zahoro alisajiliwa na Mbeya City wakati wa dirisha dogo lakini alishindwa kucheza kwa kukosa ITC ambayo ilitolewa nchini JK Kongo katika klabu ya Lupopo mwaka 2014.

Tangu mwaka 2014, amekuwa akisajiliwa na timu lakini hakufanikiwa kucheza kutokana na sakata lake la Lupopo kukata kutoa kibali cha kuachiwa kwa ITC yake.

Wiki iliyopita, rais wa TFF, Jamal Malinzi aliaahidi kulishughulikia suala lake ndani ya siku saba na kufanikiwa kutimiza ahadi hio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *