Yanga yatoa neno kuhusu wapinzani wao Ligi ya Mabingwa

Winga wa Yanga, Issoufou Boubacar akiwatoka walinzi wa Al Ahly ( Picha Soka360)

Winga wa Yanga, Issoufou Boubacar akiwatoka walinzi wa Al Ahly ( Picha Soka360)

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga wamekiri kuiona ratiba na wapinzani wao kwenye michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Licha ya kuiona ratiba hiyo, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamesema wanaamini wanakutana mabingwa watupu kwenye michuano hiyo.

Hata hivyo kuhusu mipango ya timu hiyo kuelekea kwenye michuano hiyo bado haijapangwa kwa kuwa wanakabiliwa na michuano ya Kombe la Mapinduzi na Ligi Kuu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit ameanza kwa kuelezea ukweli wa taarifa hiyo na jinsi wanavyoichukulia.

“Nimeiona, taarifa ni za kweli. Tunakutana mabingwa (Yanga ni mabingwa wa Tanzania) mwalimu ameiona lakini mipango bado hatujaamua itajulikana baada ya kukutana” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *