Yanga wanatii sheria, wachezaji na makocha wao wote wana vibali

IMG_0067

Idara ya Uhamiaji nchini imetoa orodha inayothibitisha waajiriwa wote wa kigeni wa klabu ya Yanga kuishi na kufanya kazi nchini kihalali.

Kwa mujibu wa orodha hio ya Uhamiaji Yanga imeajiri wachezaji saba wa kigeni na makocha watatu wa kigeni na kukamilisha taratibu zote za uhamiaji, wizara ya Kazi, Ajira,Vijana na watu walemavu  na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kupatiwa vibali vyao.

Orodha hio imetolewa na afisa  wa Uhamiaji mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule na kuonesha wachezaji Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe,  Vincent Bossou, Justine Zulu wamekatiwa vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.

Pia makocha George Lwandamina na msaidizi wake Noel Mwandila pamoja na mkurugenzi wa ufundi, Hans Van Der Pluijm wana vibali vya kuishi na kufanya kazi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *