Yanga kuifuata Ihefu Mbeya Kombe la Shirikisho

Droo ya raundi ya tatu timu 32 bora ya Kombe  la Shirikisho (ASFC) imechezeshwa leo saa 5 kamili asubuhi katika studio za Azamtv.

Katika droo ya leo, imezishubudia timu za Ligi za Kuu zikicheza dhidi ya timu za Daraja ka Kwanza, Daraja la Pili na Mabingwa wa Mikoa hali inayopelekea hata mikoa isiyokua na timu za Ligi Kuu kupata uhondo huo wa burudani.

Yanga watakua ugenini kucheza dhidi ya Ihefu ya Mbeya uwanja wa Sokoine, ili Azam ikisafiri mpaka Kilombero Ifakara kwenda kuwakabiri wenyeji timu ya Shupavu FC.

Droo ya leo ikichezeshwa na wachezaji nguli wa timu ga Taifa Tanzania ( Taifa stars) na vilabu mbalimbali, Mohamed Hussein Daima ‘Mmachinga’ , Savatory Edward, Yusuph Macho na Shekan Rashid.

Michezo ya mzunguko wa tatu wa Kombe la Shirikisho itachezea Januari 31 na Februari Mosi.

Ratiba kamili ta michuano hiyo ni:

KMC FC  v Toto Africans – Chamazi, Dar
Majimaji v Ruvu Shooting – Majimaji, Songea
Njombe Mji v Rhino Rangers – Sabasaba, Njombe
Kiluvya United v JKT Oljoro – Mlandizi, Pwani
Ndanda v Biashara United – Nangwanda, Mtwara
Pamba v Stand United – CCM Kirumba, Mwanza
Polisi Tanzania v Friends Rangers – Ushirika, Moshi
JKT Ruvu v Polisi Dar – Mbweni, Dar

Ihefu v Young Africans – Sokoine Mbeya
Mwadui v Dodoma – Mwadui Shinyanga
Green Warrios v Singida United – Chamazi, Pwani
Prisons v Burkina- Sokoine, Mbeya
Kariakoo v Mbao – Ilulu, Lindi
Majimaji Rangers v Mtibwa Sugar, Ilulu Lindi
Kagera Sugar v Buseresere – Kaitaba, Bukoba
Shupavu v Azam – Mkamba Ifakara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *