Yanga kucheza mechi 4 ndani ya siku kumi, ikiwemo ya Al Ahly

img-20160207-wa0012.jpg

Kutokana na kushiriki katika mashindano matatu kwa wakati mmoja, klabu ya Yanga inakabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi nne ndani ya siku kumi.

Wakati Simba ikiendelea kujikita kileleni wenzao Yanga na Azam ratiba imeendelea kuwa ngumu kwao kutokana na mrundikano wa mechi za viporo na zile za kimataifa.

Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania (TPLB) imetoa mabadiliko ya ratiba ya ligi kuu Tanzania Bara , kwa mujibu wa ratiba hiyo Yanga itacheza Ijumaa, Jumapili na Jumatano kabla ya Kuwavaa ‘Waarabu’ Al Ahly siku ya Jumamosi tarehe 9 Aprili.

Yanga wanatarajia kushuka dimbani siku ya Ijumaa ya tarehe 1 kuwavaa Ndanda katika kombe la Azam shirikisho, na siku mbili mbele watashuka tena dimbani katika uwanja wa taifa kuwakabili Kagera Sugar siku jumapili tarehe 3 Aprili.
Baada ya hapo Yanga Itapumzika siku mbili na siku ya tatu watakutana na Mtibwa Sugar, katika mchezo unaotarajiwa kutimua vumbi tarehe 6 Aprili kunako dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Upana na ukubwa wa kikosi cha Yanga utapimwa zaidi wakati watakopkuwa na siku mbili tu za kupumzika kabla ya kuwavaa Al Ahly katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika siku ya Jumamosi ya tarehe 9 Aprili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *