Yanga kuanza na Wakomoro CAF

Yanga_Mbao

Klabu ya yanga imepangwa kuanza ugenini dhidi ya Klabu kutoka komoro ya Ngaya de Mbe katika raundi ya awali ya kufuzu Klabu bingwa Afrika mchezo unaotarajiwa kupigwa kati ya Februari 10-12, 2017.

Endapo yanga itafanikiwa kuifunga Ngaya De Mbe basi itakutana na mshindi kati ya APR Ya Rwanda na Zanaco ya Zambia kabla ya kuelekea moja kwa moja hatua ya 16 bora kwa mujibu wa utaratibu mpya wa CAF.

Endapo yanga itafanikiwa kuvukwa vikwazo hivyo viwili itakwenda hatua ya 16 bora na kisha kupangwa makundi. Utaratibu huu ni mpya tofauti na ule ambao ulizoeleka awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *