Yanga inakosa muunganiko huu kimbinu na kiufundi

Kiungo mkabaji asilia ( Tshishimbi )
Kiungo mchezeshaji mwenye uwezo wa kutoa back up kama mkabaji na mchezeshaji ( double pivot ) Thabani Scara Kamusoko.

Deep lying playmaker mwenye uwezo mzuri kutoa kombinesheni kwa viungo wa kati na mshambuliaji ( Ibrahim Ajibu )

Tatizo la mawinga limeanza kupungua kwa kukomaa kwa Pius Buswita na Emanuel Martin kikubwa ni game approach na uwezo wa kuusoma mchezo wakati mechi ikiendelea ili kujua wakati gani wachezaji ndani wafanye rotation au substitute ambayo itatoa uhai kwenye defensive patterns au offensive patterns inategemea na circumstance iliyopelekea sub.

Technically viungo waliopo wanaotengeneza kombinesheni na Tshishimbi ukimuondoa majeruhi Kamusoko ni deep lying defensive midfield. Makapu na Pato ni wazuri kuwalinda mabeki wa kati lakini uchezaji wao hauleti muunganiko wa moja kwa moja na safu ya ushambuliaji hivyo kama Tshishimbi anapangwa juu asaidie ushambuliaji ni ngumu kwa sababu ni lazima ashuke chini kusaidia ukabaji zaidi kuliko ushambuliaji. Automatically foward line inakosa link nzuri na kujikuta timu nzima inakuwa defensive.

Mathalani wengi mnamuona Rafael Daudi anapwaya kwa sababu kufa kwa kiungo cha chini kunawalazimisha AMs kufanya zaidi majukumu namba mbili kuliko jukumu namba moja .

Ukiondoa hili la game approach pia Yanga inahitaji sana kujitazama kwenye masuala ya kiufundi. Timu inaonesha kukosa fiziki ya kutosha kutunza tempo ya timu kwenye kushambulia. Mchezo wa kasi huficha madhaifu na kuwafanya wapinzani kucheza chini .

Passing

Timu inapiga sana square passes na back passes na hii inatokana na udhaifu kwenye midfield. Lazima timu ipige one-two ( give and go passes ) zenye kasi zinazohama kutoka box moja kwenda nyingine kwa kasi . Umakini huu utatokana na maandalizi kifiziki , mazoezi ya kupiga pasi kwenye kasi .

Shooting

Recently limekuwa tatizo , misimu miwili iliyopita timu ilikuwa na wapigaji wazuri wa pembeni na kati . 3 attempts one goal lakini hili kwa sasa ni nadra kuliona . Ubutuaji ni mkubwa kwa sababu mipira inafika kwenye final third si kwa mipango madhubuti tokea nyuma hivyo mtu anapiga bila kujiandaa au anapiga akishakosa sehemu ya kuupeleka mpira (Build up )

Mawazo na mtazamo wangu tu.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *