Yanga, Azam walikutana na ‘Italian job’ kwa African Lyon

Abdallah Mguhi wa African Lyon akiwania mpira na Haruna Niyonzima wa Yanga.

Abdallah Mguhi wa African Lyon akiwania mpira na Haruna Niyonzima wa Yanga.

Uwezo wa mkubwa vwa kukaba kwa nidhamu ulioiwezesha African Lyon kuwabana vigogo Azam na Yanga na pia kuigonga Simba umefananishwa na mbinu za ‘Italian Job’.

Mkurugenzi wa African Lyon, Raheem Kangezi ameuambia mtandao wa Soka360 kuwa sio kwamba timu yake haiwezi kushambulia muda wote ila walijipangia kucheza kwa mbinu maalum kuweza kuwazuia vigogo wasifurukute.

” Kocha wetu aliyepo Ureno aliwasoma sana Yanga na kutusisitiza kuwazuia hasa katika wingi ya kulia. Yanga wanatengeneza mabao mengi kutokea wingi ya kulia. Tuliingia tukilijua hilo na kuwabana. ”

Katika mechi mbili dhidi ya Azam na Yanga, wachezaji wa African Lyon walicheza kwa kukaa nyuma na kuzuia kwa nidhamu ya hali ya juu.

Wakati wakitumia muda mwingi kuzuia, silaha yao ya mashambulizi ilikuwa ni Abdallah Mguhi aliyekuwa akitokea wingi ya kushoto na kufanikiwa kumpa wakati mgumu Juma Abdul.

Naye kocha wao, Charles Otieno amesema kucheza na vigogo sharti uwaheshimu kwa kucheza kwa tahadhari kubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *