Yametimia! Simba yamtimua Omog

Kocha Joseph Omog

Uongozi wa klabu ya Simba, umeachana na kocha wake mkuu Joseph Omog raia wa Cameroon kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa ya uongozi wa Simba imesema, wamefikia makubaliano hayo na Omog kwa pande zote kurudhia juu ya usitishwaji mkataba wake wa ajira.

Kikosi cha Simba sasa kitakua chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma.

Kutumuliwa kwa Omog kunafuatia matokeo mabaya na hasa mchezo wa kombe la Shirikisho walioupoteza jana dhidi ya Green Warriors inayoshiriki ligi daraja la pili.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *