Yamemfika hapaa! Kichuya aamua kutoboa ukweli

Winga wa Simba mwenye mabao matatu msimu huu, Shiza Kichuya ameuanika ukweli juu ya maisha yake ndani ya klabu ya Simba na ligi kuu kwa ujumla hususani kwenye upande wa miundo mbinu ya nchini Tanzania.

Nyota huyo aliyesajiliwa na Simba akitokea kwenye klabu ya Mtibwa Sugar ameweka wazi kwamba hali ya viwanja nchini Tanzania ni mbaya mno hasa vile vilivyopo mikoani.

Akitilia mkazo juu ya suala hilo, Kichuya ameongeza kuwa hakuna budi kwa wahusika wa viwanja hivyo kuvifanyia marekebisho au kuvitazama upya kwa jicho la tatu.

“Hali ya viwanja vyetu bado ni tatizo, kuna baadhi ya viwanja mchezaji hadi unaogopa kucheza, inabidi tuviangalie” alisema.

Katika hatua nyingine nyota huyo alielezea hali yake ya kiafya kuelekea kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Mbao, lakini nikapona, mimi suala la nani kasema nini huwa siliangalii, ninachokiangalia ni daktari amesema nini” alisema Kichuya.

One Comment

  1. Baraka martin

    October 12, 2017 at 10:12 pm

    Kweli viwanja vihovu kabisa vya mikoani wavirekebishe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *