Willian amtaja Ronaldo na Ronaldinho kama watu waliomshawishi

Winga wa klabu ya Chelsea Mbrazil, Willian amesema kwamba anafurahia kuwepo kwenye kikosi cha Chelsea chini ya kocha wake wa muda, Guus Hiddink.

image

Winga wa Chelsea, Willian (katikati).

Nyota huyo aliyekwenye kiwango kizuri msimu huu ameuambia mtandao wa UEFA kwamba siku zote alikuwa akifurahia kuwaona Ronaldo na Ronaldinho wakiwa uwanjani hivyo basi nyota hao kusimama kama watu waliomshawishi kucheza kimafikio.

Willian ameongeza kuwa alikuwa na ndoto za kukutana na nyota hao kwa kuwa wamemshawishi kutokana na aina yao ya uchezaji.

“Siku zote nilifurahia kuwatazama Ronaldo na Ronaldinho; walikuwa ni wachezaji ambao niliota kukutana nao. Wamenishawishi sana hasa kwa aina yangu ya uchezaji” alijibu Willian baada ya kuulizwa kuhusu mchezaji aliyemshawishi wakati akikua.

“Bila malalamiko. Siku zote ninajaribu kucheza kwa furaha”  aliongeza Willian baada ya kutupiwa swali jingine.

UEFA ilimuuliza kuwa kucheza huku akiwa na furaha amejifunza akiwa Brazil? Kwa kuwa siku zote ameonekana kucheza akiwa na furaha usoni.

“Uwanjani tunasahau yote yaliyotokea nje ya uwanja. Ninajitahidi kufokasi sana na yote niyafanyayo. Ninafikiri hiyo ni kwa mchezaji kukamilika uwanjani huhitaji kuwa na furaha.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *