Weah amualika Wenger kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwake

Rais mteule wa Liberia George Weah amemtumia mualiko wa kuhudhuria tukio la kuapishwa kwake kocha wa Arsenal mzee Arsene Wenger.

Hata hivyo Wenger amesema huenda asiweze kuhudhuria kutokana na kuwa busy kikazi, lakini ataweza kwenda Liberia endapo FA watamfungia kwa kitendo cha kuwasema marefa kutokana na baadhi ya maamuzi ambayo hayakumfurahisha Wenger hivi karibuni.

Weah na Wenger walifanya kazi pamoja katika klabu ya Monaco, wakati Mzee Wenger alipokuwa akiifundisha timu hiyo kuanzia 1988 mpaka 1992.

Rais mteule wa Liberia anatarajiwa kuapishwa mwishoni mwa mwezi huu nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *