We Neymar hebu muache Coutinho aende Barcelona!

Winga wa Brazili Neymar anamshawishi kiungo nyota wa Liverpool, Philippe Coutinho kujiunga na Paris Saint-Germain badala ya Barcelona wanaomhitaji kwa udi na uvumba.

Liverpool walikataa dau nono kutoka Barcelona kwa ajili ya kiungo huyo majira ya joto, wakikataa kumuuza mchezaji wao nyota licha ya kiungo huyo kuomba kuondoka.

Miamba hao wa Hispania wanatarajiwa kumrudia tena Coutinho Januari, lakini umeibuka ushindani kutoka kwa PSG.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *