Wazee Yanga wawaangukia wachezaji wao

Yanga_MbaoHuku kukiwa na tetesi za ‘mgomo baridi’ kwa wachezaji wa Yanga baada ya kutolipwa mshahara wa mwezi Novemba, wazee wa klabu hiyo wameibuka na kutoa neno kwa wachezaji wao.

Mwenyekiti wa baraza hill, Mzee Akilimari amesema anashangaa kusikia wachezaji wakiwa na madai katika uongozi huu wa Yusuph Manji ilhali viongozi hao wakionekana kuwa na kila kitu na uwezo mkubwa kifedha.

Hata hivyo mzee huyo amewaomba wachezaji wa Yanga wawe watulivu kwani anaamini kwamba uongozi utalitatua tatizo hilo haraka iwezekanavyo.

“Niwaombe wachezaji wawe watulivu na wanapotakiwa kucheza wacheze kwa uwezo wao wote” alisema.

Hapo awali kaimu katibu Mkuu, Baraka Deusdedit alikanusha madai hayo na kusema kwamba utaratibu ndiyo umebadilika kwani hapo awali ilikuwa wakilipwa mwanzo wa mwezi.

Lakini hivi sasa utaratibu umebadilika naunarejea utaratibu uliozoeleka kwa wafanyakazi wote ambapo hulipwa mwishoni mwa mwezi baada ya kufanya kazi.

Taarifa za chini kwa chini ambazo Soka360 hazijazithibitisha ni kwamba wachezaji wa Yanga wamegomea mazoezi kwa kile ambacho kinaelezwa hawajalipwa mshahara wa mwezi uliopita yaani mwezi Novemba.

Mapema asubuhi hii, kocha mkuu wa klabu hiyo, George Lwandamina aliweka ujumbe unaoonesha uwepo wa utovu wa nidhamu kwenye kikosi hicho na kuelezea umuhimu wa nidhamu kwenye maisha ya mchezaji wa kulipwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *