Wanaume kazini! Azam yaufungia kazi ubingwa

Kikosi cha Azam kikiwa mazoezini leo Asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex. [Picha| Mtandao wa Azam]

Mara baada ya mapumziko ya wikiendi, leo Jumatatu asubuhi wachezaji wa Azam wameanza rasmi mazoezi tayari kabisa kuanza kuivutia kasi Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam siku ya Jumamosi saa 1.00 usiku.

Azam inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wake wa wikiendi iliyopita dhidi ya Mbeya City.

Timu hio mpaka sasa ipo kwenye nafasi ya nne ikiwa na pointi zake 16 sawa na Simba ambao ni vinara wa ligi hio, Yanga  na Mtibwa iliyo kwenye nafasi ya pili huku tofauti ikiwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *