Wanaongoza Ufungaji La Liga msimu huu 2017-18

Lionel Messi

Lionel Messi

Huyu ni mshambuliaji wa FC Barcelona, katika mechi 15 ambazo klabu yake imecheza mpaka sasa ameweza kufunga magoli 14. Ndio kinara wa kupachika magoli mpaka sasa katika La liga kwa msimu wa 2017-18.

Simone Zaza

Huyu ni raia wa Italia akiwemo katika kikosi kilichoshindwa kuiwezesha nchi yao kushiriki michuano ya kombe la dunia mwakani nchini Urusi. Zaza ni mshambuliaji wa Valencia ambaye mpaka sasa ameweza kutupia nyavuni goli 10 katika michezo 15. Mwanzoni mwa msimu alinukuliwa na gazeti maarufu la macca akisema msimu huu amejipanga kuchukua ufungaji bora wa La liga mbele ya Lionel Messi na Christiano Ronaldo. Ataweza ? Muda utatoa hukumu.

Cedric Bakambu

Ni raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo akiwa na umri wa miaka 26 mpaka sasa. Ni mshambuliaji wa kati wa timu ya Villarreal nchini Uhispania aliyojiunga nayo msimu wa 2015-16. Mpaka sasa ameweza kufunga magoli 9 katika msimu huu wa 2017-18 lakini katika mechi 72 alizocheza na klabu hiyo toka ajiunge nayo ameweza kufunga magoli 32. Kiasilia ni mkongoman lakini alizaliwa nchini Ufaransa.

Rodrigo

Rodrigo Moreno Machado ni muhispania aliyeianza vyema safari yake kisoka na shule za soka za klabu ya Real Madrid kabla ya kujiunga na klabu yake ya sasa Valencia. Amepita vilabu vingi kama vile Bolton Wanderers nchini England na Benfica. Hucheza kama winga wa pembeni au mshambuliaji wa kati akiwe na uwezo mkubwa sana wa kumiliki mpira, kutoa pasi na kufunga . Mpaka sasa ametupia nyavuni goli 8 akishika namba 4 katika orodha ya wafungaji katika ligi ya La liga.

 

Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *