Wababe wa Sudan wamtaka Elias Maguli kwa udi na uvumba

Elias Maguli akiwa katika mazoezi ya timu ya Taifa Stars inayojiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Chad. ( Picha Soka360/ Ibrahim Mohamed)

Elias Maguli akiwa katika mazoezi ya timu ya Taifa Stars inayojiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Chad. ( Picha Soka360/ Ibrahim Mohamed)

Klabu tajiri ya Sudan, Al Hilal imedhamiria kupata huduma za mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya Stand United baada ya kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao.

Uongozi wa klabu ya Al Hilal ambayo imekuwa ni moja ya timu zenye nafasi ya ‘kudumu’ katika hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika ulifadhaishwa mno na hatua ya kutolewa kwenye mashindano hayo msimu huu. Walitolewa na klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya na hivyo kufanya maamuzi magumu ya kuachana na wachezaji wake watatu wa kigeni, Abieku Ainosoon, Nelson Ladzagla, Souleymane Cisse.

Wakala wa Elias Maguli, Faustino Mukandila ambaye amekuwa akiwauzia wachezaji Al Hilal ameuambia mtandao wa Soka360 kuwa amefanya mazungumzo na rais wa wababe hao wa Sudan, Ashraf Al Kardinal kuhusiana na uhamisho wa Maguli.

Nashughulikia uhamisho wa Maguli kwenda Al Hilal kwenye dirisha la usajili lijalo mwezi wa sita.  Wanahitaji sana huduma zake.

Maguli amekuwa katika kiwango kizuri  msimu huu tangu atue Stand United baada ya kuondoka Simba, amefunga mabao kumi mpaka sasa licha ya kuonekana kubaniwa na kocha wake Patrick Liewig.

Pia alikuwa ni moja ya wachezaji wa Tifa Stars waliong’ara kwenye mechi dhidi ya Algeria, akifunga bao moja Dar huku bao lake lingine likikataliwa kwenye mechi ya marudiano jijini Bilda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *