Waamuzi CAF sasa kulipwa posho na Shirikisho hilo

Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Africa (CAF) Limesema Kuanzia Mwaka huu 2018 Waamuzi wote watakaopangiwa kuchezesha mechi za mashindano ya CAF watalipwa moja kwa moja na Shirikisho hilo na hii ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Rais wa CAF katika kampeni zake lengo ikiwa ni kuvipunguzia gharama za uendeshaji kwenye Shirikisho la Mpira kwa nchi husika pia wanaamini itasaidia kuzuia vitendo vyovyote vya udanganyifu vinavyoweza kufanywa kwa waamuzi.

Maamuzi hayo yamefikiwa katika Kikao cha Kamati ya utendaji wa (CAF) ikiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo ndugu Ahmad kilichoketi jana Januari 9, 2018 mjini Casablanca Morocco.

CAF pia imepitisha majina ya Manne (4 ) ya wagombea wa nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo kutoka ambapo watapigiwa kura katika mkutano mkuu wa CAF unaotarajiwa kufanyika Februari 2 ,2018 Mjini Casablanca nchini Morocco.

Waliopitishwa kugombea ni Jamal El Jaafri Raia wa Libya akiwakilisha kanda ya Kaskazini,
Augustin Senghor Raia wa Senegal akiwakilisha kanda ya Magharibi A ,Sangare raia Wa Burkina Faso akiwakilisha Kanda ya Magharibi B. Patrice Edourard Ngaissona kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati na Pierre Alain Mounguengui Raia wa Gabon wote amepitishwa kugombea kuwakilisha kugombea nafasi moja ya Uwakilishi wa kanda ya kati .

BAchir Ould Zmirli kutoka nchini Nigeria tu ndiye mgombea pekee aliyeondolewa kwenye mchakato huo kutokana na kushindwa kukamilisha maombi yake ndani ya muda uliopangwa.

Pia CAF wamepitisha Ratiba ya mashindo ya vilabu barani Afrika kwa mwaka 2018 ambayo imeshawekwa tayari kwenye tovuti ya shirikisho hilo pamoja na kupitisha maboresho machache ya Kanuni zitakazosimamia mashindano hayo ya ngazi ya vilabu .

Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji pia kimejadili na kupitisha utekelezaji wa kuanza mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mashindano ya ngazi ya vilabu kwa mwaka 2018 ambapo sasa mashindano kwa msimu ujao

CAF pia Imesema inatarajia kutuma timu ya Wataalamu kwenda kufanya ukaguzi nchini Ethiopia katika robo ya kwanza ya Mwaka 2018 ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya CHAN kwa mwaka 2020,ambayo inatarajiwa kufanyika nchini humo .

Wakati huo huo CAF imesema imekwisha toa vifaa maalumu vya kisasa vya kufuatilia viwango vya wachezaji kwa nchi 5 ambazo zimefuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia inakayofanyika mwaka huu nchini Russia huku wakipanga kufanya hivyo kwa nchi nyingine 49 zilizosalia .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *