Utamu,uchungu wa viporo, Azam kucheza Ijumaa, Jumapili na Jumatano kabla ya Kuwavaa Esperance

Azam_warming

Wakati Simba wakiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kucheza michezo mitatu zaidi ya washindani wake, Azam wanaoshikilia nafasi ya tatu wanakabiliwa na ratiba ngumu kutokana na kushiriki katika mashindano matatu.

Azam watakabiliwa na mechi nne muhimu katika mashindano matatu ndani ya kipindi cha siku kumi. Siku ya Ijumaa ya Aprili Mosi, watapambana na Prisons kuwania katika mchezo wa kufuzu kwa hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho.

Baada ya hapo, watasafiri hadi Mwanza kuivaa Toto Africans ya Mwanza katika muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara siku ya Jumapili ya tarehe 3.

Siku mbili baadaye, watarudi Dar katika uwanja wao wa Azam Complex kucheza na Ndanda katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo wanatakiwa kushinda ili kuifukuzia Simba kileleni.

Siku ya Jumapili ya tarehe 10, shughuli itahamia kimataifa wakati watakapokabiliana na wababe wa Tunisia, Esperance katika mechi ya hatua ya 16 ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Wakati huo huo, kikosi cha Azam wanatarajiwa kuingia kambini leo mchana kwenye viunga vya Azam Complex tayari kabisa kujiandaa kikamilifu kwa michezo muhimu katika ndoto zao za kubeba mataji na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

Wachezaji wa Azam ambao hawapo kwenye timu zao za Taifa walipewa mapumziko ya siku tatu baada ya mechi yao  Kombe la Shirikisho dhidi ya Bidvest ya Afrika Kusini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *