Usajili wa Yanga 2017/18: Wanaoingia, wanaobakizwa na wanaotemwa

Wakati dirisha la usajili na uhamisho wa wachezaji Ligi Kuu Tanzania Bara, tayari Mabingwa watetezi, Yanga wameanza kufanya biashara ya kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu jao.


Kipa Rostand Youthe, raia wa Cameroon aliyeichezea African Lyon msimu uliopita amekuwa mchezaji wa nne kusajiliwa na Yanga  msimu.

Usajili wa Youthe ni tafsiri ya kuachwa kwa All Mustapha aliyemaliza mkataba wake na huenda Deogratius Munishi naye asiongeze mkataba mpya.


Ibrahim Hajib ametambulishwa rasmi kujiunga na Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Simba kama mchezaji huru.


Mazungumzo kati ya Yanga na beki wake kisiki, Vincent Bossou yanaonekana kukwama na tayari viongozi wa klabu hio wameinua mikono. Bossou alijiunga Yanga mwaka 2015 akitokea ligi daraja la pili Korea Kusini.


Jezi 10 iliyokuwa ikivaliwa na mshambuliaji Matheo Anthony imekabidhiwa kwa mshambuliaji mpya Ibrahim Ajib jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kama ishara mbaya kwa Matheo ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni.


Mshambuliaji Malimi Francis Busungu ameoneshwa mlango wa kutokea baada ya kumaliza msimu kwa kucheza mechi moja tu ya ligi ambayo hata hivyo alipumzishwa baada ya dakika 32 tu za kipindi cha kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.


Kiungo mkabaji, Justine Zulu anaripotiwa kuwa mbioni kutemwa na Yanga. Zulu alisajiliwa wakati wa dirisha dogo lakini baada ya kucheza mechi 8 tu za Ligi anaonekana kutokuwa na msaada mkubwa katika kikosi cha kwanza.


Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe naye ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akifuata nyayo za Donald Ngoma.


Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga licha ya awali kuhusishwa na kusaini mkataba na klabu ya Polokwane City ya Afrika Kusini.

Donald Ngoma akiandika nakala ya mkataba wake


Beki Gadiel Michael Mbaga wa Azam anaripotiwa kumalizana na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Wakati Gadiel akiwa mbioni kutua Yanga, Mwinyi Haji amemaliza mkataba wake na haijulikani kama ataongezewa mkataba mpya.


Beki Abdallah Hajji ‘ Ninja’  kutoka Taifa Jang’ombe alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga mwanzoni mwa mwezi wa Juni.

 

3 Comments

 1. Joseph Mhagama

  July 3, 2017 at 10:59 am

  Mimi ni mpenzi wa Dar Young Africans Sports Club nataka kujua ni wachezaji gani wa kigeni wanaondoka na wapi wanaingia.

 2. Nuhu Mziwanda

  December 16, 2017 at 10:23 pm

  Nataka Majina Ya Wachezaji Walio Wasajili Dirisha Dogo

 3. Daud barnaba's

  December 26, 2017 at 4:15 pm

  poa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *