Usajili Simba, wanaoingia, kutemwa na kubakia

Hivi  sasa kelele na tetesi za  usajili zimepamba moto kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati tayari Dirisha la Usajili likiwa limefunguliwa rasmi, mchuano unazidi kuwa mkali baina ya vilabu. Mashabiki wa timu kubwa wanachonga na kutambiana.

Tunakuletea uhamisho, usajili na dili zilizokamilika Katika klabu ya Simba mpaka sasa.


Simba imetangaza kumsajili kipa wa timu ya Taifa Stars, Said Mohamed kwa mkataba wa miaka miwili. Mohamed aliwahi kuichezea Yanga kabla ya kutemwa baada ya kucheza mechi ambayo Yanga walifungwa maba0 5-0 na Simba.

Hivi Karibuni aliteuliwa kupa bora wa michuano ya kombe la Cosafa nchini Afrika Kusini.

Said Mohamed


James Kotei akiwa katika zoezi la utiaji saini pamoja na mwenyekiti wa usajili Simba, Zacharia HansPoppe.

Kiraka James Kotei ameongeza  mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya Simba.

Kotei alisajiliwa na Simba kwa mkataba mfupi wakati wa dirisha dogo la usajili mwaka jana.


Simba imetangaza kumsajili beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Hassan Mbonde kwa mkataba wa miaka miwili ili kuziba pengo la Abdi Hassan Banda anayetajwa kutimkia Afrika Kusini.


HARUNA NIYONZIMA KUTOKA YANGA


Kiungo mchezeshaji, Haruna Niyonzima amekiri kumalizana na Simba. Taarifa za uhakika zikisema viongozi wa Simba walienda Rwanda kumsainisha mkataba wa miaka miwili kwa dau la dola elfu 70


JONAS MKUDE AMEONGEZA MKATABA


Jonas Mkude

Nahodha wa kikosi cha Simba, Jonas Mkude ameongeza mkataba wa kukitumikia kikosi hicho kwa miaka 2 miwili zaidi.

Taarifa hizi zimethibitishwa na mtandao rasmi wa Simba uliomnukuu Mkude akisema,

” Ulishawaji kuona wapi mtu anakimbia nyumba yake. Mimi ninaendelea kuichezesklabu ya Simbana ninafurahia kuwa pamoja na uongozi tumefikia muafaka na sasa nimsaini ksndarasi ya miaka miwili kuendelea kuichezea klabu ya Simba”

Mkude ni kati ya wachezaji wa Simba walioicheza mechi nyingi msimu uliopita akicheza kwa zaidi ya dakika 2000 katika mechi za Ligi na kuisaidia Simba kubeba taji la Kombe la Shirikisho.


ALLY SHOMARI KUTOKA MTIBWA SUGAR


Mtibwa ni nyumba ya vipaji na kwa mara nyingine Simba imegonga hodi na kuondoka na kiungo Ally Shomari ambaye pia huchezeshwa kama beki.

Tayari kiungo huyo ametambulishwa rasmi na makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange ‘ Kaburu’ na amesaini mkataba wa miaka miwili.

Ally Shomari

 


EMMANUEL ELIASI MSEJA KUTOKA MBAO


Wakati kukiwa na tetesi za Aishi Manula kumwaga wino Msimbazi, kipa wa Mbao,  Emanuel Elias Mseja amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba.


SHOMARI KAPOMBE KUTOKA AZAM


Simba imefanikiwa kumrudisha nyumbani beki kiraka, Shomari Kapombe. Kapombe aliondoka Simba  kuelekea Ufaransa kwa makubaliano maalum ya kuuzwa baadaye lakini hakudumu na baadaye kujiunga na Azam kwa mkataba wa miaka mitatu.


JOHN BOCCO KUTOKA AZAM


Baada ya miaka mingi ya kuinyanyasa Simba uwanjani, hatimaye mshambuliaji John Bocco ametua Msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam kama mchezaji huru.

Bocco anajiunga Simva huku mshambuliaji Ibrahim Ajib akielekea kutimka na kujiunga Yanga.

John Bocco


YUSUF SELEMANI MLIPILI KUTOKA TOTO AFRICANS

Tayari ameichezea Simba katika michuano ya Kombe la SportPesa baada ya kujiunga Msimbazi akitokea Toto Africans ya Mwanza iliyoshuka daraja.


JAMAL HILAL MWAMBELEKO KUTOKA MBAO


Kwa muda mrefu ni kama Simba walikuwa na beki mmoja tu wa kushoto, Mohamed Hussein kiasi cha kutumika kila mechi hata katika mashindano yasiyo rasmi.

Msimu huu mpya, Simba imeamua kumleta Zimbwe Jr, mtu wa kumsaidia. Jamal Mwambeleko tayari amewaonesha mashabiki wa Simba kile kilichomleta Msimbazi kufuatia kupata fursa ya kutumika katika mashindano ya SportPesa.

6 Comments

 1. Midiman

  June 26, 2017 at 11:00 pm

  Viongozi Simba imalisheni pia bench la ufundi Kwa kumuongeza kocha mrundi wa mbao fc.jamaa kiufundi yuko poa ataongeza mbinu za ziada hasa ktk eneo la ushambuliaji.tumeona jinsi Mbao walivyokua wanajipanga kutafuta goli.itakua vipi kama mrundi huyo awapate wakina Boko,Okwi,Ngoma,Mavugo nk.

 2. raphael mbilinyi

  July 16, 2017 at 7:49 pm

  napenda kuwashukuru nakuwapongeza wanasimba kwa usajili mzuri walio fanya hvyo tunatarajia kupata matokeo mazr kimataifa

 3. Joel samwel

  July 17, 2017 at 7:38 am

  kama kuna uwezekano kocha wa makipa abadilishwe kwani makipa huonesha kiwango kwa mda mfupi na kupwaya, pia kipa hutumika mmoja tu karibia msimu mzima kutokana na kutokuimarishwa.

 4. Apolinary Akoyce

  July 17, 2017 at 12:47 pm

  yanga xalamu zao tu make zile tano ziko njiani

 5. Johnson Chrissogon

  July 19, 2017 at 9:59 pm

  Nadhani mwaka huu tunastahili kuwa bora mara zote

 6. Apolinary Akoyce

  July 31, 2017 at 6:23 pm

  Uongozi Simba kwa kumchua mnyarwanda Etienne kwa kuongeza ujuzi zaidi akika Simba imara mwaka huuuuuu #ameizing

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *