Uingereza kuwavaa Nigeria, Costa Rica kabla ya kuelekea Urusi

Timu ya taifa ya England almaarufu kama ‘ three lions ‘ itacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kuelekea nchini Urusi kwenye michuano ya kombe la dunia.

Mechi dhidi ya Nigeria itapigwa Junin2,2018 katika dimba la Wembley na mechi dhidi ya Costarica itachezwa tarehe 7 Juni 2018.

Southgate kocha mkuu wa England amesema mechi hizo ni kipimo tosha kwa kikosi chake hususani katika kujipima na soka la Afrika na Amerika ya kati.

” tulicheza dhidi ya Brazil tukatoka sare tasa ya 0-0 na mchezo wa Germany. Hizo zilikuwa mechi kujipima na soka la Ulaya na Amerika ya kusini. Kama timu tunahitaji kujipima kwa mifumo mingine dhidi ya soka la Afrika na Amerika ya kati ili kujiweka sawa na wapinzani wetu kwenye kundi Tunisia na Panama ” alizungumza Southgate akihojiwa na waandishi wa habari.

Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *