Tottenham v Liverpool: Rekodi mbovu ya Klopp Wembley kufikia ukomo leo? Weka mzigo Sportpesa

Gumzo kubwa kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza hii leo ni juu ya mchezo wa Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Huu ni mchezo unaotazamiwa kuwa ni mkali na wa kusisima kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili tangu kuanza kwa msimu huu huku ukweli ni kwamba rekodi ya timu zote mbili ni kielelezo kingine kinachothibitisha hali ya mchezo huu itakavyokuwa.

Katika mechi zao nne za mwisho walizocheza ugenini, Liverpool haijafungwa  dhidi ya Spurs wakishinda mara mbili na kutoa sare mbili.

Jordan Henderson anatarajiwa kuitwa tena kwenye kikosi cha Liverpool kitakachosafiri kwenda Tottenham, huyu alipumzishwa timu yake iliposhinda 7-0 dhidi ya Maribor lakini ataerjea Wembley, hii inamaanisha kuwa James Milner anaweza kuikosa mechi hii licha ya kiwango bora cha katikati ya wiki.

Jurgen Klopp hajawahi kushinda mechi ya mashindano katika Uwanja wa taifa wa Uingereza, lakini Mjerumani huyo amesisitiza kuwa hafikirii rekodi hiyo kuelekea mechi hiyo.

Kwa upande wa Liverpool mlinda mlango wake, Simon Mignolet atereja langoni na Joe Gomez anaweza kucheza katika safu ya ulinzi Jurgen Klopp anaendelea kuonesha Imani juu ya walinzi chipukizi.

Ben Davies amepona majeraha na Dele Alli amerudi baada ya kutumikia adhabu yake ya Ligi ya Mabingwa kwa Tottenham.

Mousa Dembele na Victor Wanyama wote wapo nje ya mchezo huu, huku kwa upande wa Erik Lamela ambaye pia anauguza majeraha ya nyonga anatarajiwa kuukosa mchezo huo.

Liverpool hawajafungwa katika mechi zao nne za mwisho walizocheza ugenini dhidi ya Spurs wakishinda mara mbili na sare mbili, na kuruhusu goli moja tu katika kipindi hicho huku wakifunga mara tisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *