Toto: Hatuna tahadhari yoyote, tunakwenda kucheza mpira

Kikosi cha Toto Africans

Kikosi cha Toto Africans.

Mwenyekiti wa Toto Africans, Godwin Aiko amesema kwamba hawana tahadhari yoyote kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wikiendi ijayo na kusisitiza kuwa wanakwenda kucheza mipira.

Mwenyekiti huyo amesisitiza licha ya kuwa wanashika mkia kwenye Ligi Kuu hali hiyo haiwatishi na si ‘ishu’ kwa upande wao.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, hatuna tahadhari yoyote tunakwenda kucheza mpira na kuburuza mkia siyo ‘ishu'” alisema baada ya kuulizwa wanaingiaje kwenye mchezo ujao.

Toto inashikilia mkia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kushuka dimbani mara 16 na kufanikiwa kujikusanyia pointi 12 pekee.

Timu hiyo pia imeshinda michezo mitatu, sare tatu na imepoteza michezo 10 huku ikifunga mabao tisa pekee.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *