The Bavarians wamelala mbele ya Monchengladbach, wiki ya ajabu kwa Bundesliga

image

The Bavarians wapoteza mchezo wa kwanza msimu huu.

Borussia Monchengladbach kwa Mara ya kwanza wanavunja rekodi ya Bayern Munch kwa ushindi wa mabao 3-1. Ushindi unaowaweka kwenye rekodi ya kushinda michezo 10 bila kupoteza chini ya Andre Schubert.

Laiti kama kuna ambaye angejua siku yake ya kuuaga ufalme wake wa duniani, hakuna shaka The Bavarians ungewafaa.

Frank Ribery aliyekuwa akirejea kutoka kwenye majeraha na kucheza mchezo wake wa kwanza msimu huu na wa 300 kwa Bayern  nadhani alikumbwa na maumivu mengine makali kuliko hata yale yaliyomuweka nje kwa jipindi chote hicho.

Haikuwa siku murua kwa Bayern ya Pep Guadiola, licha ya kwamba Borussia Monchengladbach ni timu ngumu ila Bayern watapaswa kujiuliza mambo kadha wa kadha.

Medhi Benatia amefanya vitu kiurahisi sana kwa mlinda mlango wa Monchengladbach kwa kupiga kichwa chepesi kufuatia krosi ya Arturo Vidal.

Siku ya kufa nyani miti yote huteleza, hakukuwa na matukio yale tuluyoyazoea kutoka kwa Robert Lewandowski.

Sikuona maajabu mapya kutoka kwa Javi Martinez, Kingsley Coman Jerome Boateng wala Philipp Lahm.

Ni dhahiri shahiri, Borussia Monchengladbach waliondoa mirija yote ya oksijeni kutoka kwenye kiungo cha Bayern kwenda sehemu sahihi za mwili wa Bavarians.

Waliwapeleka mwendo ambao haukuwa saizi yao.
Pep Guardiola atulie na timu yake bado nafasi ya kuwa mabingwa wanayo.

Siku haikuwa nzuri kwa Pep na Bayern kwa ujumla, itabidi wajilaumu wenyewe kwa akili waliyoingia nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *