TFF yatangaza vituo vya RCL na makundi yake

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza vito vinne vitakavyotumika kwa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)  inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 1- 16, 2018.

Mikoa ya Geita, Rukwa, Singida na Kilimanjaro imekua wenyeji (vituo) vya michuano ya RCL msimu huu ambapo kila kundi litakua na jumla ya timu saba na kila timu mbili za juu zitafuzu moja kwa moja kupanda Ligi Daraja la Pili msimu wa 2018/2019.

Kundi A: Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Dar es salaam 2.

Kundi B: Rukwa, Katavi, Kigoma, Tabora, Ruvuma, Songwe, Mbeya.

Kundi C: Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Dar es salaam 3.

Kundi D: Kilimanjaro, Tanga, Arusha, Manyara, Pwani, Morogoro, Dar es salaam 1.

Aidha TFF imetangaza dirisha la usajili wa RCL kuanza leo April 05, 2018 na utamalizika April 18, 2018.

TFF itapitia usajili April 18-20 na kutangaza majina ya wachezaji waliombewa usajili.

April 20-23, 2018 – kipindi cha kuweka pingamizi.

April 24, 2018 – Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kupitia usajili.

April 25-28, 2018 – Muda wa kutoa leseni za wachezaji

Mei 01- 16, 2018 kuanza na kumalizika kwa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa.

 

One Comment

  1. Pingback: TFF yatangaza vituo vya RCL na makundi yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *