TFF yapata udhamini wa kampuni ya Macron

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa udhamini wa jezi kwa timu za Taifa zote na Kampuni ya vifaa ya Macron ya Italia.

Katika mkataba huo kampuni hiyo itatoa vifaa kwa timu za vijana na wa wakubwa wa kike na kiume kwa kipinidi cha miaka miwili.

Hii ni hatua kubwa kwa soka la Tanzania na haswa TFF kupata udhamini wa kampuni kubwa kutoka Ulaya wenye udhoefu na utengenezaji vifaa vya michezo.

Kampuni hiyo itatoa fedha kiasi cha Euro 300,000 sawa na TZS 791,749,000 kwa miaka miwili.‬
‪Hongera TFF‬

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *