Tetesi za usajili dirisha dogo Ligi Kuu Tanzania Bara

Ulimwengu akiwa mazoezini Sweden.

Yanga imekanusha kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu.

Donald Ngoma anatajwa kutimkia kwenye klabu ya Singida United licha ya klabu yake ya sasa, Yanga kusema kuwa hawafahamu lolote juu ya hilo.

Azam ipo mbioni kumalizana na washambuliaji wawili kutoka nchini Zambia na Ghana ili kuziba pengo la mshambuliaji wake iliyoachana nae, Yahya Mohamed.

Simba imeambiwa kuwa haina haja ya kuongeza mchezaji yeyote kwenye dirisha hili dogo la usajili kwani ina kikosi bora.

Pastory Athanas anatajwa kurejea Stand United.

Taarifa zinaeleza kwamba, Shiza Kichuya amekataa kuongeza mkataba ndani ya klabu ya Simba baada ya kupata dili nchini Misri.

Nyota wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa Banka, anatajwa kuwaniwa kwa udi na uvumba na klabu ya Yanga licha ya mwenyewe kukanusha na kusema hafahamu lolote.

 

4 Comments

 1. Menase kibiki

  November 17, 2017 at 9:30 am

  Huyo ngoma siaende jamani maana anatusumbua sana anajiona yeyeendoyeye

 2. SAIMON

  November 20, 2017 at 7:19 pm

  ngoma asepe zake tu.

 3. Joel samwel

  November 21, 2017 at 8:31 am

  mwacheni kichuya aende akaoneshe kiwango chake nje, lakini ibrahimu’mo’ asiondoke kwenda yanga hawana lolote

 4. Given

  November 30, 2017 at 3:54 pm

  kichuya so wakucheza tanzania saiz yule n wa nche 2 naitwa Given wimile wa ikelu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *