Tetesi za usajili barani Ulaya leo Jumatatu

Real Madrid ipo tayari kuweka mezani kitita cha pauni milioni 200 kumng’oa mshambuliaji wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari.

Rais wa Klabu ya Real Madrid, Florentino Perez malengo yake makubwa ni kumsajili Eden Hazard kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi yajayo licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa klabu yake ya Chelsea.

Manchester City wanatarajia kumpatia mkataba mpya Raheem Sterling baada ya nyota huyo wa timu ya taifa ya Uingereza kuonesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu.

Juventus wanaihitaji saini ya nyota wa Liverpool, Emre Can ili kukiimarisha zaidi kikosi chao.

Real Madrid inataka kumuuza nyota wake Gareth Bale baada ya kuonekana kukabiliwa na majeraha ya muda mrefu huku timu inayohitaji huduma yake itatakiwa kuweka mezani kitita cha pauni milioni 85.

David Moyes amemhakikishia nyota Javier Hernandez kuendelea kusalia kwenye kikosi cha West Ham.

Everton na Leicester City zimeingia kwenye vita kali ya kumuwania nyota wa New York City, Jack Harrison huku dau lake likitajwa kuwa ni pauni milioni 6.

Arsenal inahitaji kumsajili Wilfried Zaha kwa dau la pauni milioni 35 ili kuchukua nafasi ya Alexis Sanchez kama ataondoka kikosini hapo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *