Tetesi za usajili barani Ulaya leo Jumatano

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amewapa makavu Manchester City baada ya kusisitiza kuwa  watampambana kutomuuza Alexis Sanchez kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu Uingereza. Wenger amesisitiza kumbakiza Sanchez anayetaka kuondoka Emirates.


Kipa Gianluigi Donnarumma, 18, amesaini mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuichezea AC Milan hadi mwaka 2021.


Eric Dier wa Tottenham amewaambia washkaji zake kuwa anataka kujiunga na Manchester United. Amewataarifu kuwa anafurahia uwezekano wa kufanya kazi chini ya Jose Mourinho anayetajwa kuwania saini yake.

Eric Dier


Adnan Januzaj anaelekea kutimka Manchester United kwa jumla kufuatia kuwa karibu kumalizana na Real Sociedad.


Borussia Dortmund wako tayari kumuachia mshambuliaji wao, Pierre-Emerick Aubameyang kutua Chelsea kwa dau la pauni milioni 65.


Manchester United ipo katika mchakato wa kumnasa Ivan Perisic wa Inter Milan kabla ya ziara yao ya China wiki ijayo. Dau la Perisic linakadiriwa kuwa pauni milioni 49.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *