Tetesi za usajili barani Ulaya leo Jumanne

Nyota wa Ivory Coast na PSG, Serge Aurier anaripotiwa kufikia makubaliano ya kujiunga na Manchester United.

Beki huyo wa kulia ataongeza ushindani wa namba katika kikosi cha Jose Mourinho.


Liverpool imeendelea kumtolea macho Virgil van Dijk wakati Southampton ikijiandaa na maisha bila ya nyota wake huyo kwa kutoa ofa ya pauni milioni 12 kumpata Wesley Hoedt wa Lazio.


Mpango wa Arsenal wa kupunguza kikosi chake umecheleweshwa na wachezaji kugoma kuhamia timu nyingine kwa maslahi madogo.


Kiungo wa Manchester United, Marouane Fellaini atafikiria mustabali wake mwezi Januari baada ya kuwasili kwa Nemanja Matic kutoka Chelsea.

Fellaini anatakiwa na Galatasary lakini Jose Mourinho amesema hana mpango wa kumuuza.


Diego Simeone amedokeza huenda Diego Costa akajiunga na Atletico Madrid mapema Januari wakati klabu hio itakuwa imemaliza adhabu ya kutosajili.


Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp aesema Philippe Coutinho hauzwi licha ya kudaiwa kumpigia hesabu Renato Sanches kama mtu sahihi wa kuziba pengo la mbrazil huyo kama ataondoka Anfield.


Kocha wa Newcastle, Rafael Benitez anaweza kumkosa Andreas Samaris kwa sababu ya matatizo ya fungu la usajili.


Manchester United ipo katika vita na Arsenal na Tottenham kwa ajili ya kumgombea kinda wa Manchester City, Jadon Sancho


Bofya hapa kupata odds kubwa zaidi za SportPesa

One Comment

  1. Anwar

    August 3, 2017 at 9:17 am

    Mnafanya kazi nzuri sana vijana wangu.kunyweni mirinda nyeusi hapo naja kulipia.I’m out.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *