Tetesi za usajili barani Ulaya leo Ijumaa

David Moyes anatarajiwa kumuacha Marko Arnautovic alieonesha kiwango duni msimu huu baada ya meneja huyo kuwashiwa taa ya kijani na West Ham ya kuhakikisha anamuondoa kikosini mchezaji yeyote mwenye kiwango cha chini.

Frank Lampard amekataa katakata uwezekano wa kurejea Chelsea kuchukua nafasi ya Michael Emenalo.

Nyota wa Barcelona, Javier Mascherano ameweka wazi dhamira yake ya kutaka kuihama klabu hio na kutimkia kwenye timu ya River Plate.

Joleon Lescott amempigia chapuo mlinzi wa Manchester United John Stones kwamba ni bidhaa yenye kiwango cha juu kwenye soko la usajili.

Dau la uhamisho la pauni milioni 53 huenda likavunja mkataba wa Samuel Umtiti kwenye klabu ya Barcelona baada ya Manchester United kuonesha nia ya kumuhitaji.

Pep Guardiola amerejesha majeshi yake kwenye klabu ya Arsenal kwa nguvu zote ili kuhakikisha inamg’oa Alexis Sanchez.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *