Tetesi za usajili barani Ulaya leo Alhamisi

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho yupo mbioni kusaini dili jipya la kuendelea kusalia klabuni hapo kwa miaka mitano mingine huku akivuta kitita cha Paundi milioni 65.

Barcelona wazifufua mbio zao za kumuwania Philippe Coutinho huku taarifa zikieleza kwamba kitita cha Paundi milioni 120 huenda kikamng’oa nyota huyo kwenye klabu ya Liverpool mwezi Januari.

Harry Kane atajwa kuendelea kusalia kwenye klabu ya Tottenham lakini kama kuna klabu itaweka mezani kitita cha Paundi milioni 200 huenda nyota huyo akauzwa.

Mesut Ozil huenda akasalia Arsenal kutokana na kutojitokeza timu yoyote kuonesha nia ya kumlipa mshahara wa Paundi 330,000 kwa wiki.

Huenda Real Madrid ikamruhusu nyota wake Gareth Bale kujiunga na Manchester United kwa kitita cha Paundi milioni 89 huku ikimuwinda nyota wa Spurs Delle Alli.

David Silva ameongeza mkataba wa kuendelea kusalia Manchester City mpaka mwaka 2020 huku akivuta kitita cha Paundi 150,000 kwa wiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *