Tathmini: Stand Utd v African Sports

Nani kutoka kuzimu?
Timu hizi zinakutana zikiwa na matokeo mabaya. Zote hazijaonja ladha ya ushindi kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.

Stand United inayodhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ilianza vibaya kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar. Katika mchezo wa pili, ilichezea tena kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam.

Kwa vyovote vile Stand United itajitahidi kuvuna alama tatu kuepuka kuwakatisha tamaa mashabiki wake msimu ukiwa bado mchanga.

Kocha mfaransa, Patrick Liewig hana budi kushinda pambano hili ili kurudisha matumaini na imani ya mashabiki na viongozi wa timu hio wanaoota mafanikio ya haraka haraka kutokana na kuwa moja ya timu zenye udhamini mzuri kwa sasa.

Mabadiliko makubwa yaliyotokana na msukumo mkubwa wa mashabiki kuhoji upangaji wa kikosi ulimfanya kocha Patrick Liewig afanye mabadiliko makubwa 7 kwenye kikosi kilichoanza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kwa upande wa African Sports, kipigo cha tatu mfululizo kitafanya maisha ya Ligi Kuu kuwa magumu Zaidi kwao. Wakati ubingwa ni ndoto kwao, hesabu za kubaki Ligi Kuu zishaanza na sare au ushindi ugenini kwa timu kama Stand United ndio ‘haba haba hujaza kibaba’ zinazoweza kuwa salama kwa upande wao.

Kikosi cha Stand United kilichonyukwa na Azam: Mohamed Makaka, Revocatus Richard, Abuu Ubwa, Rajab Zahir, Hamad Ndikumana, Hassan Dilunga, Pastory Athanas ( Kheri Khalifa 82’) , Suleiman Selembe (Erick Kayombo 51’) , Hassan Seif (Elias Maguli 69’) , Haruna Chanongo, Jacob Masawe.

Mechi za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara jumamosi hii

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *