Tambwe ndani, Kavumbagu atoswa kikosi cha Burundi

Tambwe_Dribble

Mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga amejumuishwa katika kikosi cha timu yake ya Taifa ya Burundi inayojianda kwa ajili ya mchezo wa Kundi Kkufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017 dhidi ya Namibia.

Wakati Tambwe akitarajiwa kuondoka leo kujiunga na wachezaji wenzake wa Burundi, mshambuliaji wa Azam Didier Kavumbagu hajajumuishwa katika kikosi hicho.

Kavumbagu ambaye amekuwa na msimu usio mzuri mpaka sasa alikuwa akisumbuliwa na majeruhi yaliyomweka nje kwa muda katika klabu yake ya Azam.

Burundi ina pointi tatu ikishika nafasi ya pili nyuma ya vinara Senegal katika mbio za kusaka tiketi moja ya kufuzu kwa fainali zitakazofanyika nchini Gabon.

Intamba Murugamba wataanzia nyumbani katika Uwanja wa Prince Prince Louis Rwagasore  jijini Bujumbura siku ya Jumamosi  kabla ya kurudiana Jumanne Uwanja wa Sam Nujoma Stadium , jijini Windhoek.

Kikosi kamili:

Walinda lango: Arakaza Mac Arthul,  Rugamadiye Yvan, Nzokirantevye Jeff

Walinzi na viungo:  Harerimana Rachid Léon, Kiza Fatak, Nizigiyimana Karim, Nshimirimana David,  Hakizimana Issa,  Barenge Pistis, Ndikumana Yussuf Lule ,Mustapha Francis ,Nahimana Shassir ,Tokoto Andre , Hakizimana Djuma ,Tonto Shabani ,Hussein Attaquants ,Ndarusanze Claude, Ndikumana Selemani

 

Washambuliaji: Nduwarug Christophe , Nsabiyumva Frederic, Harerimana Hafizi, Tambwe Amissi, ( Yanga, Tanzania) , Laudit Mavugo,  Papy Faty ( Bidvest Wits, Afrika Kusini),  Pierrot Kwizera,(Rayon, Rwanda) Ndabashize Dugaly, Cedrick Amissi, Fiston Abdoul Razak,( Bloemfontein Celtic, Afrika Kusini), Abassi Nshimirimana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *