Taifa Stars kufanya kama Serengeti Boys leo?

Timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, leo inatarajiwa kushuka dimbani kuwavaa Angola katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Cosafa linaloendelea nchini Afrika Kusini.

Hii itakuwa ni karata ya pili kwa Taifa Stars baada ya kufanikiwa kuanza vizuri kwa kuwachapa Malawi 2-0 siku ya Jumapili.

Tanzania na Angola zinakutana ikiwa ni takriban mwezi mmoja tangu timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys kuwafunga wenzao wa Angola mabao 2-1 katika mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17.

Matokeo ya ushindi wa aina yoyote yataipa Tanzania tiketi ya kufuzu robo fainali kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki michuano hio mwaka 1997.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *