Straika Mtanzania atua kwa Mabingwa wa Botswana

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Mtibwa Sugar, Rashid Mandawa ametua nchini Botswana kujiunga na mabingwa nchi hio, Township Rollers.

Mandawa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya Jumanne tayari kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia klabu hio inayojiandaa kutetea taji lake la Ligi Kuu Botswana na pia kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Msimu ulioisha Mandawa aliifungia Mtibwa Sugar mabao nane katika Ligi akiwa amesajiliwa kutoka Mwadui aliyodumu nayo kwa msimu mmoja akitokea Kagera Sugar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *