Stewart Hall awapa dole Azam

Stewart Hall

Stewart Hall

Kocha mkuu wa klabu ya AFC Leopards, Stewart Hall amezungumzia kufukuzwa kwa benchi la ufundi la klabu yake ya zamani ya Azam.

Katika mazungumzo na mtandao wa Soka360, Hall amefurahishwa na uamuzi wa kumrejesha Kally Ongala kuchukua mikoba ya Wahispania.

” Ni maamuzi sahihi, nadhani Kally atawafaa sana, namuunga mkono. ”

Hall alimsajili Kally kama kocha-mchezaji pamoja na kumpa majukumu ya ukocha msaidizi kabla ya wote kuondoka baada ya Kally kuamua kwenda kusomea ukocha Uingereza huku Hall akijiuzulu.

Katika mazungumzo ya huko nyuma na mtandao wa Soka360, Hall alisema anaumizwa mno na matokeo mabovu ya Azam kwani ni timu ambayo anaipenda na yuko tayari kurudi kuifundisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *