Stewart Hall amteua kocha Mtanzania kuwa msaidizi wake Kenya

Denis-Kitambi

Dennis Kitambi, wa kwanza kushoto akiwa katika benchi la ufundi la Azam

Kocha wa zamani wa Azam, Stewart Hall ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha timu ya AFC Leopards ya Kenya, leo amemteua Dennis Kitambi kuwa msaidizi wake.

Kwa uteuzi huo, Kitambi anakuwa kocha msaidizi wa AFC Leopards ambayo inajipanga upya kurudi katika ubora wake baada ya kuyumba sana msimu huu.

AFC Leopards Ilichukua ubingwa wa Kenya kwa mara mwisho mwaka 1998 ilipokuwa ikifundishwa na kocha Mtanzania, Sunday Kayuni.

 

Kitambi alianzia ukocha katika klabu ya Ndanda aliyofanikiwa kuipandisha Ligi Kuu kabla ya kuachana nayo na kujiunga na katika benchi la ufundi la Azam.

Katika klabu ya Azam, Kitambi alianz kufanya kazi kama msaidizi wa George Best Nsimbe aliyekaimu nafasi ya ukocha mkuu baada ya kutimuliwa kwa Joseph Omog. Baada ya Hall kurudi Azam kwa mara ya tatu aliungana na Kitambi na kujenga uhusiano mkubwa wa kikazi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *