Stars kutua nchini usiku mnene!

Mara baada ya kwenda sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Benin usiku wa jana kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea nchini mapema usiku wa kuamkia kesho, Jumanne.

Kikishawasili nchini Tanzania, kikosi hicho kitavunja kambi yake ili kupisha ratiba nyingine ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania, Alfred Lucas amethibitisha juu ya taarifa hio.

“Timu inatarajiwa kuwasili nchini usiku wa kuamkia kesho, Jumanne yaani itaingia majira ya saa tina na nusu usiku, ikishawasili kambi itavunjwa ili kupisha ratiba za ligi kuendelea,” alifafanua Alfred Lucas.

Katika hatua nyingine Lucas amesema kwamba kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 kinaendelea na kambi yake jijini Dar es Salaam chini ya kocha wake Oscar Miranbo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *