Sportpesa yazindua kituo kikubwa cha huduma kwa wateja

Dar es Salaam, Tanzania –Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa leo February 1, imezindua rasmi kitengo cha huduma kwa wateja ili kuendelea kuboresha huduma zao.

SportPesa kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Utawala na Udhibiti, Ndugu Tarimba Abbas, imeujulisha umma kuwa kitengo maalum cha huduma kwa wateja, kilikuwa kikiendesha shughuli zake nchini Kenya ambapo ndipo yalipo makao makuu ya kampuni hiyo.

“Ili kuboresha zaidi huduma zetu tumehamishia kitengo chetu cha huduma kwa wateja katika ofisi zetu za hapa Dar es Salaam ili kuonyesha ni jinsi gani tunawajali na kuwafikiria wateja wetu kwa kusogeza huduma karibu yao.

“Kutokana na moja ya changamoto ambazo vijana wanapitia kuwa ni ajira, sisi kama SportPesa tumeajiri vijana wapatao 84 kwenye kitengo chetu na vijana hawa wamefanyiwa mafunzo jinsi ya kuwasikiliza na kuwahudumia wateja kwa uzoefu wa hali juu.

“Kama mnavyojua sisi tutakuwa ni kampuni ya kwanza ya michezo ya kubashiri yenye huduma kwa wateja wake saa 24 siku 7 za wiki, hii inaonyesha ni namna gani mteja wetu ni kipaumbele namba moja”, alifafanua Ndugu Abbas.

Wateja wa SportPesa wanaweza kuendelea kuwasiliana na huduma kwa wateja saa 24 kila siku kupitia nambari 0764 115588, 0692 115588 na 0685 115588 kwa msaada Zaidi.

Mkurugenzi huyo aliwaomba watanzania kuendelea kuiunga mkono kampuni hiyo ambayo imedhamiria kuleta sura mpya kwenye sekta ya michezo nchini sambamba na kubadilisha maisha ya mtanzania mmoja mmoja kupitia program mbalimbali ikiwa ni pamoja na promosheni ya siku 100 ya TVS KING DELUXE ambayo inatarajia kufika tamati siku ya kesho.

SportPesa ndio mdhamini mkuu wa vilabu vya Simba na Yanga pamoja na Singida United kwa nchini Tanzania na sasa wako ukingoni mwa promosheni yao ijulikanayo kama SHINDA NA SPORTPESA ambapo washindi 100 wa bajaji aina za TVS KING wamepatikana katika promosheni hiyo na kuweza kubadili maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *